Medical OPD Clinic
Posted on: December 21st, 2024TAARIFA FUPI JUU YA KLINIK YA MOYO NA SUKARI:
- Katika hospitali ya Mkoa wa Tabora –KITETE kuna aina mbalimbali za klinik zinazofanyika miongoni mwa kliniki hizo ni pamoja na kliniki ya moyo pamoja na sukari.
- Kliniki ya moyo hufanyika kila siku ya jumanne ya kila wiki ambapo wagonjwa wote wenye matatizo ya moyo huonwa na daktari maalum katika kliniki hiyo.
- Kliniki ya Ugongwa wa kisukari hufanyika kila siku ya alhamisi ya kila wiki ,ambapo pia Daktari maalum hukaa na kuwaona wagonjwa hao.
- Kliniki hii inafanya kazi kwa wiki mara mbili kama ilivyoainishwa hapo huu isipokua siku za mapumziko maalum ya kiserikali.
- Kliniki hii inaona wagonjwa wa aina zote ,Wagonjwa wanaotumia bima,wagongwa wanaolipia huduma papo kwa papo na pia wale ambao hutibiwa kwa msamaha kwa mujibu wa sheria.
- Katika kliniki yetu wagonjwa wote ni sawa,fika upate huduma iliyo bora
- Imeandaliwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya ndani
Dkt.Nassoro I. Kaponta.